Ripoti dukuduku lako
English | Français | Kreyòl Ayisyen | Español | ภาษาไทย | नेपाली
Shirika la kimataifa linalohusika na masuala ya uwajibikaji ‘Accountability Counsel’ limejikita katika kutekeleza majukumu yake kwa uadilifu wa kiwango cha juu, likizingatia taaluma na maadili, kwa kuheshimu haki, na maslahi ya mashirika tunayoshirikiana nayo yanayofanya kazi katika jamii tunazozihudumia.
Ikiwa unachochote kuhusu kazi yetu, au taarifa zozote kuhusu ukiukwaji wa sera zilizoainishwa hapo chini, tunakuhimiza kuwasilisha taarifa hiyo hapa kwa kutumia fomu hii. Taarifa zote zitachukuliwa kwa uzito unaostahili. Unaweza kuwasilisha taarifa yako kwa siri. Hatutambagua wala kumdhuru mtu yoyote atakeyewasilisha taarifa kwetu.
Taarifa zinazohusiana na dukuduku lililowasilishwa na hatimaye usimamizi wa kesi zitatunzwa kwa usiri na usalama wakati wote na kushirikishwa kwa wale tu ambao ni wahusika muhimu katika kusimamia kesi husika. Shirika la ‘Accountability Counsel’ litahakikisha kuwa ripoti za siri na taarifa nyingine za kina kuhusu ukiukwaji wa sera zinatunzwa na kuhifadhiwa kwa usiri na usalama.
Maelezo zaidi kuhusu sera zetu yanaweza kupatikana hapa:
- Sera ya Kupambana na Utumwa na Usafirishaji Haramu wa watu
- Sera ya ulinzi wa mtoto
- Sera ya kukubali zawadi na mapato
- Kanuni za maadili ya mawakili wa kimataifa
Ikiwa una maswali yoyote kuhusu sera hizi, tafadhali wasiliana nasi kwa barua pepe ethics@accountabilitycounsel.org Mkurugenzi wetu wa Fedha na Utawala pamoja na Mkurugenzi Mtendaji watapokea barua pepe hizo.